IQNA

Washindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Huduma kwa Qur'ani waenziwa

17:06 - July 31, 2012
Habari ID: 2381820
Washindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Huduma kwa Qur'ani Tukufu jana usiku walienziwa na kutunukiwa zawadi katika sherehe maalumu zilizofanyika huko katika mji wa Jeddah Saudi Arabia.
Sherehe hizo ambazo zilifanyika kwa usimamizi wa Mfalme Abdul Aziz wa nchi hiyo zilihudhuriwa na wataalamu, watafiti na wakuu wa vituo vya Qur'ani vya Saudia ambavyo vinafungamana na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani Tukufu.
Akizungumza katika sherehe hizo, Abdallah Basifr, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo amesema tuzo hiyo hutolewa kwa watu ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kufundisha na kuhudumia Qur'ani Tukufu. Baadhi ya watu na taasisi zilizotunukiwa tuzo hiyo ni pamoja na chuo bora zaidi cha Qur'ani Tukufu, mashindano bora zaidi ya Qur'ani, Jumuiya bora zaidi ya hifdhi ya Qur'ani, kituo bora zaidi cha hifdhi ya Qur'ani, madrasa bora zaidi ya hifdhi ya Qur'ani, kipindi bora zaidi cha Qur'ani katika televisheni, tovuti bora zaidi ya Qur'ani, msomaji mzee bora zaidi wa Qur'ani duniani na mtafiti bora zaidi wa mafunzo ya Qur'ani.
Kuarifishwa juhudi kubwa zaidi zilizofanyika kwa ajili ya kuhudumia Qur'ani duniani, kuandaliwa uwanja mzuri kwa ajili ya mashindano ya wahudumu wa Qur'ani, kuenezwa taasisi za Qur'ani na mbinu za ufundishaji Qur'ani Tukufu pamoja na uwezeshaji wa hifdhi ya Qur'ani ni miongoni mwa malengo ya kutolewa tuzo hiyo. 1066242
captcha