IQNA

Mashindano ya kimataifa ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yafanyika Pakistan

17:08 - July 31, 2012
Habari ID: 2381824
Mashindano ya kimataifa ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yalifanyika jana Jumatatu huko Islamabad mji mkuu wa Pakistan kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la Daily Times, mashindano hayo yameandaliwa na Baraza la Sanaa la Rawalpindi kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Islamabad. Vitengo tofauti vya chuo kikuu hicho pia vimeshiriki katika uandaaji wa mashindano hayo. Nchi tofauti za Kiislamu zimeshiriki katika mashindano hayo.
Washiriki wa Pakistan na Saudi Arabia ndio waliochukua nafasi za kwanza na pili za mashindano hayo.
Rahman Aswi, mkuu wa kitengo cha lugha ya Kiarabu katika chuo kikuu kilichotajwa alizungumza mwishoni mwa mashindano hayo na kusema Qur'ani Tukufu ambayo ndio msingi wa kubuniwa sheria katika jamii za Kiislamu imeleta mabadiliko makubwa duniani. Amesisitiza kwamba mafundisho ya Qur'ani ndiyo suluhisho bora zaidi la kutatuliwa matatizo na changamoto mbalimbali zinazomkabili mwanadamu wa leo.
Mzungumzaji mwingine katika mashindano hayo alikuwa profesa Manur Gandal mkuu wa kitengo cha lugha na fasihi ambaye alisema kwamba Waislamu wanapasa kufanya juhudi maradufu za kusoma, kutafakari na kutekeleza mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu maishani. 1066936
captcha