Mashindano hayo ambayo ni ya 31 ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani yalianza Jumapili iliyopita yakiwashirikisha makarii na mahafidhi 179 kutoka miji mbalimbali ya Guinea.
Mkurugenzi taifa wa Jumuiya ya Masuala ya Kiislamu ya Guinea Conakry Bala Diane alisema katika sherehe ya kufungua mashindano hayo kwamba anatarajia kuwa mashindano hayo yatakuwa hatua muhimu ya kuwahamasisha wanafunzi wa shule na vyuo vikuu vya nchi hiyo kutilia maanani utamaduni wa Qur'ani Tukufu.
Mashindano hayo yatamalizika tarehe Agosti katika sherehe itakayohudhuriwa na viongozi wa kiserikali na kidini. 1067212