Shirika la habari la Malaysia Bernama limeripoti kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo amesema lengo hilo ni tukufu na kuongeza kuwa taasisi husika zinapaswa kufanya juhudi za kushika nafasi ya pili katika uchapishaji wa nakala nyingi zaidi za Qur'ani duniani.
Razaq Tun ambaye alikuwa akizungumza katika sherehe za kuzindua tarjumi mpya ya Qur'ani tukufu amesema kuwa ataunga mkono juhudi za kufikiwa lengo hilo tukufu.
Katika sherehe hiyo kumezinduliwa chapa ya tarjumi mpya ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kimalai. 1067415