IQNA

Nusu fainali ya mashindano ya kiraa ya Qur'ani inafanyika Ufaransa

20:03 - August 01, 2012
Habari ID: 2383387
Nusu fainali ya mashindano ya kiraa ya Qur'ani Tukufu inafanyika leo nchini Ufaransa.
Mashindano hayo ambayo duru zake za awali zilifanyika tarehe 12, 13 na 14 Julai yanafanyika leo katika Studio Raneem nchini Ufaransa yakiwashirikisha watu 16.
Awamu hii ya mashindano ya kiraa ya Qur'ani inafanyika katika makundi mawili ya vijana wenye umri wa chini na zaidi ya miaka 16 na wengi waliofaulu kuingia nusu fainali walikuwa wasichana wa Kiislamu.
Jumuiya ya Waislamu wa Ufaransa ambayo ndiyo inayosimamia mashindano hayo imetangaza kuwa mashindano hayo yatarushwa hewani moja kwa moja na redio ya Pastel FM kwa ushirikiano wa kituo cha Raneem.
Washindi wa mashindano hayo watapewa zawadi nono ikiwa ni pamoja na kudhaminiwa gharama za safari ya kwenda umra huko Saudi Arabia. 1068368

captcha