Abdul Qadr Sarhan, mkuu wa idara inayosimamia mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Misri amesema Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo inajiandaa kuandaa duru ya 20 ya mashindano hayo.
Sarhan amesema mashindano hayo yamepangwa kuanza Jumatatu tarehe 6 Agosti kwa kuwashirikisha washindani 87 kutoma Misri na nchi nyingine 61 za dunia. Amesema mashindano hayo yatafanyika kwa uungaji mkono wa Rais Muhammad Mursi wa Misri na kwa ushirikiano wa Kituo cha Kiislamu cha al-Azhar.
Mashindano hayo ambayo huandaliwa nchini humo kila mwaka na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri yamepangwa kuendelea hadi tarehe 16 mwezi huu.
Sarhan amebainisha kuwa lengo la kuandaliwa mashindano hayo ni kuwashajiisha vijana katika ulimwengu wa Kiislamu kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu pamoja na kuelewa maana ya aya zake. Mashindano hayo yatafanyika katika makundi matano ya hifdhi ya Qur'ani nzima kwa kuchunga sheria za tajwidi na tartili pamoja na tafsiri ya juzuu ya nne ya Qur'ani, hifdhi ya Qur'ani nzima na kuchunga sheria za tajiwidi na tartili, hifdhi ya juzuu 20 za mwanzo za Qur'ani sambamba na kuchunga sheria za tajwidi na tartili, hifdhi ya juzuu 10 za mwanzo za Qur'ani sambamba na kuchunga sheria za tajwidi na tartili na hatimaye hifdhi ya juzuu 6 zinazofuatana za Qur'ani Tuufu.
Kundi la tano la mashindano hayo litawahusu washindani ambao lugha ya si Kiarabu na wasiokuwa wanafunzi wa al-Azhar.1069518