Khatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran, Ayatullah Ahmad Jannati amesema kuwa, lengo la mashinikizo na njama za Magharibi na baadhi ya nchi za eneo hili la Mashariki ya Kati dhidi ya serikali ya Syria ni kulinda uwepo wa Uzayuni na kuiondoa Damascus katika uwanja wa kuunga mkono muqawama wa Palestina.
Ayatullah Ahmad Jannati ameashiria kuwepo njama za Wamagharibi na kushiriki baadhi ya nchi za eneo hili katika njama za kuharibu usalama na utulivu nchini Syria na kusisitiza kuwa, kinachowafanya maadui wasimame pamoja dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu ni uungaji mkono wa Syria kwa muqawama sambamba na kujaribu kuuokoa utawala haramu wa Israel ambao unaelekea kusambaratika.
Aidha Khatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema, uingiliaji wowote katika masuala ya ndani ya nchi nyingine ni kinyume kabisa na sheria za kimataifa na ni jambo lisilokubalika. Ameongeza kuwa, Marekani, Saudia Arabia, Uturuki na Qatar zinapaswa kukomesha mara moja uingiliaji wao katika masuala ya Syria.
Katika upande mwingine Ayatullah Ahmad Jannati aneashiria lengo la kushadidishwa vikwazo vya kisiasa na kiuchumi vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, Marekani inakusudia kulidhoofisha kiuchumi taifa la Iran ili kwa njia hiyo Washington iweze kuitawala tena Iran.
Amesema wananchi wa nchi hii wanapaswa kuwa macho sambamba na kuzuia njama chafu za mabeberu dhidi ya Iran ya Kiislamu. 1069566