IQNA

Maonyesho ya kwanza ya Qur'ani ziliazoandikwa kwa mkono yafunguliwa Tunisia

17:45 - August 04, 2012
Habari ID: 2385254
Maonyesho ya kwanza ya nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za mkono yalifunguliwa jana Ijumaa katika Maktaba ya Taifa ya Tunisia kwa hima ya mwambata wa kiutamaduni wa Iran.
Baada ya kufunguliwa maonyesho hayo kwa kiraa ya msomaji wa kimataifa wa Iran Hassan Ridhaiyan, mkuu wa Maktaba ya Taifa ya Tunisia aliishukuru Iran kwa ushirikiano mzuri katika kuanzisha maonyesho ya nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za mkono.
Amesema kuwa nakala 37 za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za mkono ambazo baadhi yao ziliandikwa katika karne ya 2 na 4 zinaonyeshwa kwenye maonyesho hayo. Amesema 21 kati ya nakala hizo zimetoka katika Maktaba ya Taifa ya Iran na 16 zilitoka kwenye Maktaba ya Taifa ya Tunisia.
Mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Tunisia Sadiq Ramadhani pia amesema kuwa jumba la makumbusho la Maktaba ya Taifa ya Iran iko tayari kupanua zaidi ushirikiano wa kiutamaduni na taasisi husika hususan Maktaba Kuu ya Tunsia. 1070154

captcha