IQNA

Msaada wa familia, jambo muhimu katika mafanikio ya hifdhi ya Qur'ani

17:03 - August 05, 2012
Habari ID: 2386099
Ahmad Taha, mwakilishi ya Palestina katika duru ya 16 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Dubai Imarati amesema kwamba uungaji mkono na msaada wa familia ni suala muhimu katika mafanikio ya kuhifadhi Qur'ani Tukufua.
Taha ambaye ni mwanachuo wa taaluma ya tiba katika Chuo Kikuu cha al-Quds na mwakilishi wa Palestina katika mashindano yaliyotajwa amesema licha ya kuwa baadhi ya familia hazilipi umuhimu suala la kuwafundisha watoto wao Qur'ani Tukufu lakini baadhi yao hutoa umuhimu mkubwa kwa suala hilo.
Amesema kama haungekuwa msaada wa wazazi wake wawili na hasa baba yake mzazi ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu kilichotajwa, hangefikia mafanikio aliyofikia katika suala la kuhifadhi Qur'ani. Hafidh huyo aliye na umri wa miaka 20 na ambaye alianza kuhifadhi kitabu hicho cha mbinguni akiwa na umri wa miaka 18 alifanikiwa kukihifadhi chote katika kipindi cha mwaka mmoja.
Anasema alikuwa akihifadhi kuraza 12 kila siku na kurejea kile alichokuwa amekihifadhi kila baada ya siku tatu. Ameendelea kusema kwamba mwanzo alianza kuhifadhi Qur'ani akiwa peke yake lakini baadaye akaendelea kukihifadhi kwa kunufaika na msaada wa familia yake pamoja na walimu mujarabu wa Qur'ani.
Baada ya kufanya vyema katika mashindano kadhaa ya kitaifa Ahmad Taha baadaye aliteuliwa kuiwakilisha nchi ya Palestina katika mashindano ya kimataifa ya Dubai.
Hafidh mwingine wa Qur'ani Tukufu ambaye anasisitiza juu ya mchango wa familia katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu ni Ya'qub Adam, mwakilishi wa Chad katika mashindano hayo na ambaye ana umri wa miaka 18. Amesema Baba yake ni mwalimu wa Qur'ani ambaye amemsaidia sana kuhifadhi kitabu hicho cha wahyi. Alianza kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka 13 na kuikamilisha akiwa na miaka 15.
Ameongeza kuwa alikuwa akihifadhi kurasa mbili kila siku na kurejea kile alichokuwa amehifadhi kila baada ya siku moja. 1071078
captcha