Sheikh Muhammad ambaye alitangaza uamuzi wake wa kukubali madhdhebu ya Ahlul Bait hivi karibuni katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq amesema Waislamu wa madhehebu yote ya Kiislamu wanapaswa kushikamana na kuwa na umoja kwa sababu wao wote ni Waislamu na wafuasi wa Mtume Muhammad (saw).
Amesema kuwa anapinga mgawanyiko wa aina yoyote kati ya Waislamu na Waislamu wanapaswa kuelewa kwamba maadui wanataka kuzusha hitilafu kati yao.
Sheikh Sankoh Muhammadi hivi karibuni alitangaza kwamba amekubali madhehebu ya Ahlul Bait katika mji mtakatifu wa Karbala akiwa na umri wa miaka 68.
Sheikh Sankoh ambaye kiasili ni mtu wa Cameroon anaishi nchini Ufaransa tangu miaka 43 iliyopita. 1071407