IQNA

Mashirika ya masuala ya kheri yashukuriwa katika mashindano ya Qur'ani ya Dubai

17:57 - August 06, 2012
Habari ID: 2386984
Mashirika ya Mambo ya Kheri yamesifiwa na kushukuriwa katika usiku wa kumi wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea huko Dubai kutokana na huduma zao muhimu kwa umma wa Kiislamu.
Licha ya kuwa kuna nchi 88 zinazoshiriki katika mashindano hayo lakini ni wawakilishi wa nchi 22 tu ndio walioshiriki mashindano ya jana yaliyohudhuriwa na watu wachache sana.
Sababu ya suala hilo imetajwa kuwa ni wakati mrefu wa kufanyika mashindano hayo na pia kufanyika kwa kuchelewa yaani saa nne usiku hadi saa nane usiku wa manane na pia kiwango cha juu cha joto. Licha ya kuwa jamii ya Dubai inazingatia sana Qur'ani lakini idadi ndogo ya watu wanaohudhuria mashindano hayo imewavunja moyo washindani na kuwafanya wasishiriki kwa hamu katika mashindano hayo.
Jambo jingine ambalo limewashangaza watu ni udhaifu mkubwa wa wawakilishi wa Imarati katika mashindano hayo. Licha ya kuwa nchi hiyo ndiyo mwenyeji wa mashindano hayo lakini hadi sasa haijawasilisha washindani wowote wa maana wanaoweza kupata nafasi nzuri kwenye mashindano hayo. 1071865
captcha