IQNA

IQNA yapongezwa kwa kuakishi mashindano ya Qur’ani Dubai

13:34 - August 07, 2012
Habari ID: 2387424
Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa IQNA limepongezwa kwa kuwa chombo cha habari kilichoakisi kwa njia bora zaidi Mashindano ya 16 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu Dubai.
Katika sherehe iliyofanyika Jumatatu usiku Agosti sita, Ibrahim Bu Melha, Mwenyekiti wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai alipongeza juhudi za IQNA katika kuakisi habari za mashindano hayo. Amemtunuku Cheti cha Heshima mwandishi wa IQNA aliyeakisi mashindano hayo.
Bu Melha hasa amepongeza hatua ya IQNA kuakisi habari za mashindano hayo kwa lugha muhimu za dunia.
Mashindano ya Kimataifa ya Qurani Dubai hufanyika kila mwaka kwa hisani ya Shaikh Mohammad Rashid Al Maktoum, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu ambaye pia ni Mtawala wa Dubai.
Mashidano hayo yatamalizika tarehe 20 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo Yusuf Estes anatazamiwa kutunukiwa tuzo ya Shakhsia wa Kiislamu wa Mwaka. Ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na juhudu zake za kueneza mafundisho ya Kiislamu katika nchi za Magharibi.
1072901
captcha