IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya wanachuo Waislamu ni muhimu kwa umma

13:13 - August 07, 2012
Habari ID: 2387467
Maadui wanatekeleza njama nyingi dhidi ya umma wa Waislamu duniani na kwa hivyo kuna haja ya kuandaa hafla za kidini na Qur’ani kama vile Mashindano ya Kimataifa ya Qurani ya Wanachuo Waislamu ili kukabiliana na njama hizo.
Hayo yamesema na Ziyadullah Rahman Quelv mwakilishi wa Tatarstan katika kitengo cha qiraa katika Awamu ya Nne ya Mashindano ya Kimataifa ya Qurani ya Wanachuo Waislamu.
Katika mahojiano na IQNA amesema mashindano hayo yataonyesha umoja na mshikamano wa umma wa Waislamu.
Ameongeza kuwa wanachuo vijana kutoka kote duniani watakutana katika amshindano hayo kama familia moja ambapo wataonyesha ujuzi wa ustadi wao katika fani ya kusoma na kuhifadhi Qur’ani.
Qarii Rahman Qulev ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuandaa mashindano hayo na ameelezea matumaini yake kuwa mashindano hayo ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili yatafanyika kila mwaka katika siku za usoni.
Tatarstani ni jamhuri katika Shirikisho la Russia.
Mashindano ya 4 ya Kimataifa ya Qur'ani Maalumu kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (wanachuo) yatafanyika kuanzia Septemba 12 hadi 16 mwaka huu wa 2012 katika mji wa Tabriz nchini Iran.
1066372
captcha