IQNA

Duru ya 20 ya Mashindano ya Qur'ani Tukufu yafunguliwa Misri

13:20 - August 07, 2012
Habari ID: 2387619
Duru ya 20 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ilifunguliwa leo Jumanne mjini Cairo Misri.
Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo yamefunguliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na Ahmad Tayyib Sheikh wa al-Azhar pamoja na Tal'at Ufeifi, Waziri wa Wakfu wa Misri.
Chuo cha al-Azhar kinashirikiana na pande husika katika kuandaa mashindano hayo ambayo yanawashirikisha zaidi ya washindani 90 kutoka Misri na nchi nyingine 61 za dunia.
Waziri wa Wakfu wa Misri amebainisha namna mashindano hayo yatakavyofanyika na kuongeza kuwa washindi wa makundi yote matano ya mashindano hayo yanayotazamiwa kukamilika tarehe 26 Ramadhani wataenziwa na kutunukiwa zawadi katika wiki ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Amesema lengo kuu la mashindano hayo ni kuwashajiisha vijana wa ulimwengu wa Kiislamu kuzingatia zaidi usomaji, hifdhi na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Waziri wa Wakfu wa Misri amesema washiriki wa mashindano hayo pia watapewa fursa ya kuyatembelea maeneo ya kidini na kiutamaduni ya Misri.
Zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mashindano hayo zimetajwa kuwa za thamani ya juneih laki 6 za Misri. 1072019
captcha