Sherehe hizo ziliandaliwa na Wizara ya Sheria, Masuala ya Kiislamu na Wakfu ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Wasat linalochapishwa nchini humo sherehe hizo zimefanyika katika msikiti mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Ahmad Fatih kwa ushirikiano wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Bahrain na kwa usimamizi wa mfalme wa nchi hiyo.
Kabla ya hapo kulifanyika duru ya 17 ya mashindano hayo ya kitaifa iliyojumuisha makundi tofauti ya hifdhi ya Qur'ani nzima, hifdhi ya juzuu 20, juzuu 10, juzuu 5, juzuu 3 na kiraa kwa sauti za kuvutia maalumu kwa wanafunzi.
Wizara ya Sheria Masuala ya Kiislamu na Wakfu ya Bahrain iliwaalika wananchi wote wa nchi hiyo kuhudhuria sherehe hizo kama njia ya kuwashajiisha mahafidh na makarii wa Qur'ani kushiriki zaidi katika mashindano yajayo ya Qur'ani. 1072294