Tamasha hilo lililowashirikisha wanaharakati wanawake wa Sudan wanaojishughulisha na masuala mbalimbali yanayohusiana na Qur'ani Tukufu kutoka katika pembe mbalimbali za nchi hiyo, lilikamilika hiyo juzi kwa kutolewa hutuba mbalimbali.
Wafumaji wa mavazi yanayokwenda sambamba na mafundisho ya Kiislamu pamoja na wasanii wanaohudumia Qur'ani ni miongoni mwa watu walioenziwa na kutunukiwa zawadi katika tamasha hilo.
Nafi' Ali Nafi', naibu mkuu wa chama tawala aliyezungumza katika sherehe ya ufungaji wa tamasha hilo amesema serikali ya Sudan inazingatia sana suala la hifdhi ya Qur'ani na kuhudumia kitabu hicho cha wahyi na kwamba wananchi wa nchi hiyo pia wana nafasi muhimu katika uwanja huo.
Akisisitiza udharura wa kutafakari na kuzingatia ujumbe wa kitabu hicho, Ali Nafi' amesema Qur'ani ni kitabu cha malezi kwa mwanadamu na wala si cha kusomwa na kuhifadhiwa tu bila kufanyia kazi mafundisho yake.
Tunaashiria hapa kwamba tamasha hilo limeandaliwa na Sekritarieti ya Masuala ya Wanawake ya chama tawala cha Congress ya Kitaifa kwa usimamizi wa Ali Uthman Muhammad Taha, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan. 1072344