IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur’ani Dubai kumalizika leo

15:39 - August 08, 2012
Habari ID: 2388674
Mashindano ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur’ani Tukufu Zawadi ya Dubai yanamalizika leo.
Sherehe za kufunga mashindano hayo ambayo ni makhsusi kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 21 itahudhuriwa na Waziri Mkuu ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Muhammad bin Aal Maktoum, wawakilishi na mabalozi wa nchi za Kiislamu.
Sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Yusuf Stas, mhubiri wa Kiislamu wa Marekani ambaye amesilimu na kukubali dini ya Kiislamu hivi karibuni. Stas ameteuliwa kuwa shakhsia wa Kiislamu katika mwaka huu wa 2012.
Karii Muhammad Jawad Muhammadi wa Iran mwenye umri wa miaka 19 ambaye pia anashiriki katika mashindano hayo anatazamiwa kuwa miongoni mwa wasomaji bora wa Mashindano ya Qur’ani Zawadi ya Dubai.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Zawadi ya Dubai hufanyika kila mwaka kuanzia Ramadhani 1 hadi 20. Wiki ya kwanza ya mashindano hayo huwa ya vikao na makongamano na mashindano yenyewe ya Qur’ani huanza rasmi tarehe 8 Ramadhani.
1073635



captcha