IQNA

Kikao cha masuala ya kiufundi cha Waandishi wa Qur'ani katika maonyesho ya Tehran

15:41 - August 08, 2012
Habari ID: 2388675
Kikao cha masuala ya kiufundi cha Waandishi wa Qur’ani Tukufu kitafanyika Ijumaa ijayo katika chumba cha Darur Kitab katika Maonyesho ya Kimataifa ya 20 ya Qur’ani Tukufu mjini Tehran kikihudhuriwa na waandishi hodari wa nakala za Qur’ani.
Kikao hicho kitakachoanza jioni kitachunguza kanuni za uandishi wa nakala za Qur’ani Tukufu. Vilevile kikao hicho kitawaenzi waandishi hodari wa nakala za Qur’ani ambao wamefanya jitihada kubwa katika uwanja huo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran yalianza tarehe 15 Julai na yatamalizika tarehe 14 Agosti. 1074145
captcha