IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya al Aqsa yaanza Palestina

15:40 - August 08, 2012
Habari ID: 2388677
Mashindano ya Kimataifa ya Hifdhi na Kiraa ya Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la al Aqsa yalianza Jumatatu ya wiki hii katika mji wa Ramallah huko Palestina.
Gazeti la al Quds linalochapishwa Palestina limeripoti kuwa mashindano hayo yanawashirikisha makumi ya makarii na mahafidhi wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali duniani chini ya usimamizi wa Kamati ya Majaji kutoka nchi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu.
Mashindano hayo yataendelea hadi mwishoni mwa wiki hii na yanafanyika katika sehemu tatu za hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na tajwidi, hifdhi ya juzuu 20 pamoja na tajwidi na hifdhi ya juzuu 10 pamoja na tajwidi.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya al Aqsa yatakamilika kwa sherehe maalumu na kutolewa zawadi kwa washindi.
Mkurugenzi wa kitengo cha hifdhi ya Qur'ani katika Wizara ya Wakfu ya Palestina Sheikh Taysir al Rajabi amesema katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo kwamba lengo lake ni kuanzisha ushindani kati ya wanaharakati wa Qur'ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kuimarisha ushirikiano baina ya Waislamu kutoka pembe mbalimbali duniani, kuwahamasisha kuzuru Msikiti wa al Aqsa na Quds Tukufu ili wajionee kwa karibu jinai za utawala ghasibu wa Israel na kuweka wazi jinai hizo. 1073791

captcha