Kwa mujibu wa gazeti la Daily Times, wakuu wa maonyesho hayo wanasema kuwa lengo la kufanyika kwake ni kuhuisha thamani za mwezi mtukufu wa Ramadhani kupitia maonyesho hayo ya sanaa ya Qur'ani na vilevile kunyanyua kiwango cha kaligrafia nchini humo.
Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa maonyesho hayo, Muhammad Shueib Shafi, naibu mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Tiba cha Pakistan amesema wasanii wa kaligrafia ya Qur'ani kwa hakika ni walinzi wa turathi za Kiislamu.
Waqar Ahmad, msimamizi wa Baraza la Sanaa la Rawalpindi pia amezungumza katika maonyesho hayo na kusema kuwa kutokana na kuwa waandishi wa mkono wa Qur'ani wana nafasi muhimu katika Uislamu, lengo la maonyesho hayo ni kuhuisha sanaa kongwe ya Kiislamu na taaluma za kaligrafia.1074160