IQNA

Qur’ani ndio inayoweza kuunganisha Waislamu

6:11 - August 09, 2012
Habari ID: 2388794
Waziri wa Wakfu wai Misri Tal’at Afifi amesema Qur’ani Tukufu ndio mhimili wa umoja wa Waislamu na chimbuko la heshima ya umma wa Kiislamu.
Akizungumza katika sherehe za kufungua Mashindano ya 20 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu mjini Cairo amesema, ‘Tunapaswa kurejea katika Qur’ani na kujenga upya thamani na misingi yetu kwa msingi wa Neno la Allah.’
Amesema historia inaonyesha kuwa kila wakati Waislamu wanaporejea katika mafundisho ya Qur’ani wanapata hadhi na heshima duniani na kila wakati wanapoiacha Qur’ani wanapata matatizo na masaibu.
Mashindano ya 20 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu mjini Cairo yalianza Jumatatu Agosti 6 na yanawashiriki makarii na mahafidhi kutoka nchi 65. Mashindano hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Muhammad Abdu katika Chuo Kikuu cha Al Azhar na yataendelea hadi tarehe 26 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani (Agosti 15)
Mashindano hayo yana vitengo vya hifdhi kwa kuzingatia kanuni za tartil na tajwidi.
1073308
captcha