IQNA

Iraq yatoa stempu ya kumbukumbu kwa Maadhimisho ya Miaka 1,500 Tangu Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW)

18:37 - September 11, 2025
Habari ID: 3481215
IQNA – Msimamizi wa haram ya Hazrat Abbas (AS) huko Karbla, Iraq ametangaza kutolewa kwa stempu maalum ya kumbukumbu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 1,500 tangu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Stempu hiyo imetolewa kwa ushirikiano na Wizara ya Mawasiliano ya Iraq, ikiwa ni sehemu ya Tamasha la Kimataifa Rahmah lil-Alamin (Rehema kwa Walimwengu).

Tamasha hilo, lililoandaliwa na haram hiyo, lilianza tarehe 8 Septemba 2025, sambamba na tarehe 15 ya Rabi’ al-Awwal, na limedumu wa siku tatu, kwa mujibu wa taarifa ya Al-Kafeel.

Sayyid Ridwan al-Salami, Naibu Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kiutamaduni na Kifikra katika haram hiyo, alisema kuwa uratibu rasmi unaendelea na Wizara ya Mawasiliano ili kukamilisha taratibu za idhini, uchapishaji, na usambazaji wa stempu hiyo katika nchi kadhaa kama toleo la kimataifa.

“Lengo la stempu hii ni kuandika tukio la kihistoria la kuzaliwa kwa Mtume na kulihifadhi katika kumbukumbu ya kitamaduni na vyombo vya habari kupitia chombo chenye thamani ya urithi na utamaduni,” alisema al-Salami.

Aliongeza kuwa juhudi hii ni sehemu ya shughuli pana za kiutamaduni za haram hiyo zinazolenga kuadhimisha matukio ya kidini na kihistoria, pamoja na kuongeza uelewa kuhusu ujumbe na dhamira ya Mtume Muhammad (SAW)..

3494541

 

captcha