Haya ni kwa mujibu wa Ali Javad kutoka Uholanzi ambaye katika mahojiano na IQNA amesema waandalizi wa mashindano hayo ya Qur’ani wanapaswa kuzingatia suala hilo.
Javad ambaye atawakilisha Uholanzi katika Mashindano ya 4 ya Kimataifa ya Qur'ani Maalumu kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu yatakayofanyika Iran amesema kati ya mambo yanayopaswa kuzingatia ni kuwapa pointi zaidi washiriki kutoka nchi zisizo za Kiislamu. Qarii huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema alianza kusoma Qur’ani akiwa na umri wa miaka minane.
Javad amesema kutokana na kupotoshwa ukweli kuhusu Uislamu, Qur’ani na Waislamu katika nchi za Magharibi kuna haja ya Waislamu waishio katika nchi hizo kutekeleza kikamilifu mafundisho ya Kiislamu ili waweze kuwa kigezo chema.
Mashindano ya 4 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (wanachuo) yatafanyika kuanzia Septemba 12 hadi 16 mwaka huu wa 2012 katika mji wa Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran.
1068517