IQNA

Wanawake Waislamu Tanzania washiriki katika programu ya Qur’ani

6:08 - August 09, 2012
Habari ID: 2388797
Kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Chuo cha Kidini cha Darul Huda mjini Dar es Salaam Tanzania kimenadaa programu maalumu ya Qur’ani kwa ajili ya wanawake.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, programu hiyo inajumuisha dua za kila siku za mwezi wa Ramadhani ambazo zinasomwa na Sheikh Hussein Shahidi katika chuo cha kidini cha Darul Huda. Aidha wanazuoni wa kidini wanatoa hotuba za kidini kuhusu Sira na fadhila za Mtume SAW na Ahul Bait AS pamoja na masuala mengine yanayohusu mwezu mtukufu wa Ramadhani.
Washiriki aidha wanasoma juzuu moja ya Qur’ani Tukufu kila siku na wanashiriki katika sala za jamaa ndani ya chuo hicho.
Chuo cha kidini cha Darul Huda mjini Dar es Salaam kinatoa mafunzo ya Kiislamu na Qur’ani kwa wasichana na wanawake Waislamu.
1070058
captcha