IQNA

Tafsiri ya sura ya Anfal kutolewa katika Chuo Kikuu cha London

17:11 - August 11, 2012
Habari ID: 2390314
Tafsiri ya sura ya Anfal ya Qur'ani Tukufu imepangwa kutolewa Septemba Mosi katika Chuo cha Queen Mary kinachofungamana na Chuo Kikuu cha London.
Kwa mujibu wa tovuti ya iidr, kikao cha tafsiri hiyo itakayochambua pande mbalimbali za sura ya Anfal kimepangwa kuanza saa 3 na kuendelea hadi 12 na nusu jioni. Kikao cha kutafsiri sura hiyo ambayo ilimteremkia Mtume (saw) baada ya ushindi wa Waislamu katika vita vya Badr kitachambua sababu za ushindi wa Waislamu na ahadi za Mwenyezi Mungu kwa waumini katika vita hivyo.
Kikao hicho kimeandaliwa na Chuo cha Utafiti wa Kiislamu cha Uingereza BAQS. Chuo hicho ambacho kinafungamana na Taasisi ya Kiislamu ya Utafiti na Ustawi IIDR kilianzishwa kwa lengo la kujishughulisha na utafiti wa masuala ya Qur'ani na hadi sasa kimekuwa kikiandaa vikao vya mafunzo, semina za Qur'ani, kutoa mafunzo kwa walimu wa Qur'ani, kuchapisha makala za kiutafiti kuhusu Qur'ani na kuimarisha masomo ya Qur'ani Tukufu kupitia mtandao.
Chuo hicho hutoa mafunzo ya muda mfupi ya kuijua Qur'ani na tafsiri za sura tofauti za kitabu hicho kitakatifu. 1075654
captcha