IQNA

Mashindano ya Qur'ani yafanyika katika televisheni ya Tunisia

17:05 - August 11, 2012
Habari ID: 2390316
Televisheni ya al-Wataniya1 ya Tunisia imefanya jambo lisilo la kawaida nchini humo kwa kurusha hewani moja kwa moja mashindano ya Kiraa ya Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Tekiano, katika mashindano hayo ambayo hufanyika kila siku ya Jumatano, washiriki 6 walio na umri wa chini ya miaka 20 hushindana moja kwa moja katika usomaji wa Qur'ani na kisha waamuzi kutoa maoni kuhusiana na usomaji wao.
Baada ya hapo watazamaji pia hupewa fursa ya kutoa maoni yao kuhusiana na washindi wa mashindano hayo kupitia ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.
Kila wiki washindi wawili huchaguliwa kuwa washindi ambapo wamepangiwa kushiriki katika mashindano ya mwisho yatakayofanyika tarehe 27 ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Washindi watatu wa kwanza watachaguliwa na watazamaji wa televisheni hiyo kwa njia hiyo hiyo ya SMS.
Mashindano hayo yalianza mwanzoni mwa mwezi huu wa Ramadhani. 1075848
captcha