Sherehe hizo zilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu wa Senegal Sheikh Ahmad Salum na wawakilishi na nchi za Mauritania, Burkina Faso, Sierra Leone, Togo, Guinea Conakry na Guinea Bisssau.
Mashindano hayo ya kieneo ya Qur'ani Tukufu yamekuwa yakifanyika nchini Senegal tangu mwaka 1993 yakisimamiwa na Jumuiya ya Vijana Waislamu ya Senegal na taasisi nyingine za kidini katika mwezi wa Ramadhani.
Katika hotuba yake kwenye sherehe hizo Sheikh Ahmad Salum amesema madrasa za Qur'ani nchini Senegal zinakabiliwa na tatizo kubwa na kwamba serikali ya Dakar inapaswa kuunda wizara au taasisi huru ya kushughulikia matatizo hayo. 1075687