Taarifa iliyotolewa na mbunge huyo imesema nakala hizo za Qur'ani ina juzuu 28 tu na ina kasoro ya juzuu mbili za Qur'ani Tukufu.
Amesisitiza kuwa nakala hizo elfu 40 za Qur'ani zimechapishwa katika kiwanda cha uchapishaji cha al Tawfiqiyya chini ya usimamizi wa Sheikh Ahmad al Nasrawi ambaye ni miongoni ma mashekhe wa chuo cha al Azhar. Ameongeza kuwa makosa hayo ni makubwa kiasi kwamba hayaweza kufumbiwa macho na ni ya makusudi.
Wakati huo huo Spika wa Bunge la Misri Ahmad Fahmi amewasilisha suala hilo kwa Sheikh wa al Azhar Ahmad al Tayyib na Kamati ya Fatuwa ya Misri na kuwataka kufuatilia suala hilo kwa bidii. 1074961