IQNA

Masomo ya Qur'ani Tukufu kufunzwa katika shule za umma Senegal

19:05 - August 12, 2012
Habari ID: 2391126
Wizara ya Elimu ya Senegal imetangaza kuwa kuanzia mwakani itaanza kutoa masomo ya Qur'ani Tukufu katika shule zote za umma nchini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Lesoleil, Ibrahim Swal Waziri wa Elimu wa Senegal aliyekuwa akizungumza jana Jumamosi katika hadhara ya walimu wa Qur'ani, amesema kuwa serikali ina nia ya kutoa mafunzo ya kidini na hasa maosomo ya Qur'ani Takatifu katika shule zote za serikali za nchi hiyo.
Amesema mbali na masomo ya misingi ya Uislamu, kiraa, hifdhi na tafsiria Qur'ani Tukufu masomo kuhusu dini nyingine za mbinguni pia yatatolewa katika shule hizo.
Waziri Swal amesema masomo hayo yatakuwa ya lazima ili kuwawezesha wanafunzi kujua misingi ya Uislamu na dini nyinginezo za mbinguni.
Waziri wa Elimu wa Senegal amesema mwishoni mwa hotuba yake kwamba shule za Qur'ani yaani madrasa zina nafasi muhimu katika kueneza mafunzo ya dini ya Kiislamu miongoni mwa wanafunzi na kwamba wanafunzi ambao hawajabahatika kusoma kwenye madrasa hizo hawapasi kunyimwa fursa ya kusoma Qur'ani. 1076366
captcha