Kwa mujibu watovuti ya IIU kongamano hilo litaandaliwa na wanachama wa kundi la Jamhuri la Pakistan, Kundi la Tafsiri na Tarjumi la Chuo cha Lugha na Fasihi ya Kiarabu na Kundi la Tafsiri na Taaluma ya Qur'ani la Chuo cha Utafiti wa Kiislamu kinachofungamana na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Islamabad nchini Pakistan.
Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kuchunguza matatizo yanayoambatana na tarjumi za Qur'ani Tukufu katika lugha mbalimbali za dunia.
Masuala kama vile historia ya tarjumi ya Qur'ani katika eneo la mashariki mwa Asia na matatizo yaliyomo katika tarjumi za Qur'ani zilizotajumiwa kwa lugha mbalimbali za eneo hilo pamoja na athari zake ni baadhi ya masuala yatakayochunguzwa katika kongamano hilo.
Wanachuo, wahadhiri wa vyuo vikuu, watarjumi mashuhuri wa Qur'ani Tukufu pamoja na wataalamu wanaojishughulisha na masuala mbalimbali ya Qur'ani wamealikwa kushiriki kwenye kongamano hilo. Mijadala ya kongamano hilo itaendeshwa kwa lugha tatu za Kiurdu, Kiarabu na Kiingereza. 1076015