Sherehe hizo zilizofanyika leo saa 12 jioni kwa wakati wa Tehran zimehudhuriwa na viongozi wa masuala ya kiutamaduni na Kiislamu nchini.
Kitengo hicho cha kimataifa kilifunguliwa Jumatatu Julai 30 ambapo wasanii, wasomi, wanazuoni, wataalamu na watafiti wa masuala ya Kiislamu na Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali za dunia wamekua wakikitembelea na kunufaika na masuala tofauti yanayoonyeshwa na kuendeshwa katika kibanda hicho.
Kitengo hicho kilichoendesha shughuli zake kwa muda wa siku 10 kimewezesha washiriki wa maonyesho hayo kuwasilisha vitabu, mabango na kazi tofauti za mikono zinazohusiana na Qur'ani Tukufu. 1076673