Vyombo hivyo vimeitaka Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Algeria kuchukua hatua za lazima kwa ajili ya kushughulikia suala hilo, baada ya kutolewa ripoti kuhusiana na kusambazwa kwa nakala hizo zilizo na upungufu wa sura na vilevile kufutwa baadhi ya aya zake katika miji kadhaa muhimu ya nchi hiyo.
Sura zilizofutwa katika nakala hizo za Qur'ani ni pamoja na Ibrahim, Hijr na Nahl na pia makosa mengi ya kimaandishi na maneno yanaonekana katika baadhi ya nuskha hizo.
Vyombo vya habari vya Algeria vimesikitishwa sana na uzembe wa maafisa wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya nchi hiyo na kutumai kwamba maafisa hao wataondokana na usingizi wao wa kughafilikia suala hilo muhimu na kuchukua hatua za lazima ili kuzikusanya nakala hizo zote zilizo na kasoro.
Inasemekana kuwa nakala hizo zimekuwa zikitawanywa katika misikiti ya nchi hiyo baada ya kuidhinishwa na wizara hiyo, jambo ambalo limezidisha hasira ya wananchi Waislamu wa nchi hiyo. 1076618