Kituo cha habari cha On Islamu kimeripoti kuwa kampeni za uchaguzi wa rais wa Marekani uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu zinaandamana na wimbi jipya la uhasama na propaganda chafu dhidi ya Waislamu.
Michele Bachmann ambaye hadi mapema mwaka huu alikuwa miongoni mwa wagombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican amepinga suala la Waislamu kupewa nafasi za uongozi katika serikali ya Marekani na kulitaja suala hilo kuwa ni kupenya kwa fikra za Kiislamu katika serikali ya nchi hiyo. Vilevile amemtuhumu msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Huma Abedin kuwa ni kibaraka wa makundi ya Kiislamu.
Wanasiasa hawa wa Marekani wamekuwa wakifanya kila wawezalo kuhakikisha kwamba Waislamu hawashirikishwi katika masuala ya kisiasa na kijamii ya Marekani. Wanasiasa wenye misimamo hii ya kupiga vita Uislamu ambao wamezidisha propaganda zao chafu dhidi ya dini hiyo na wafuasi wake katika kipindi hiki cha kukaribia uchaguzi wa rais nchini Marekani wamekuwa wakichochea fikra za wananchi suala ambalo limezidha chuki na uhasama dhidi ya wafuasi wa dini hiyo.
Takwimi zilizotolea na Baraza la Uhusiano wa Kiislamu na Marekani (CAIR) na Chuo Kikuu cha California zinaonesha kuwa, fikra za kuwatisha watu wa Marekani kuhusu eti 'hatari Uislamu' zinaenea kwa kasi kubwa.
Jamii ya Waislamu nchini Marekani inakadiriwa kuwa na zaidi ya watu milioni 7. 1076035