IQNA

Ayatullah Fadhil Musawi:

Imam Sadiq (as) amekutambua kuwa mbali na Qur'ani kuwa ndiyo sababu kuu ya hitilafu zilizopo kati ya Waislamu

11:14 - August 13, 2012
Habari ID: 2391604
Katika haditi zake nyingi Imam Ja'far Swadiq (as) amekutambua kuwa mbali na Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume (saw) kuwa ndiyo sababu kuu ya mifarakano na hitilafu zilizopo kati ya Waislamu na aliona kwamba iwapo Waislamu watarejea katika Qur'ani na Suna basi hitilafu na migawanyiko yao itapungua sana.
Hayo yanesemwa na Ayatullah Sayyid Fadhil Musawi al Jabiri, mhadhiri wa elimu ya fiqhi na usuli katika Chuo Kikuu cha Kidini cha Najaf huko Iraq. Amesema kuwa hadithi zilizopokewa kutoka kwa Imam Sadiq zinaonesha kuwa, alikutambua kuwa mbali na Qur'ani na Suna za Mtume kuwa ndiyo sababu kuu ya kujitokeza hitilafu kati ya Waislamu.
Amehoji kuwa ni kwa nini sisi Waislamu tonahitilafiana? Je, hii si kwa sababu tumekuwa mbali na Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume (saw)? Amesisitiza kuwa hapana shaka kwamba iwapo tutarejea katika vyanzo hivyo viwili vya umoja na mashikamano tutaona jinsi hitilafu zilizopo kati ya Waislamu zitakavyopungua kwa kiwango kikubwa na kufikia daraja ya chini kabisa.
Ayatullah Musawi al Jabiri amesema, Imam Sadiq (as) aliwataka Waislamu kushikamana na Qur'ani na Suna za Mtume na Ahlibaiti zake watoharifu kwa ajili ya kujenga umoja na mshikamano kati yao kwa sababu Mtume (saw) amesema katika hadithi ya Thaqalaini kwamba iwapo Waislamu watashikamana na Qur'ani na Ahlul Bait basi hawatapotea.
Amesema Ahlul Bait wanaielewa vyema zaidi Qur'ani kuliko sisi na suala hilo limeashiriwa sana katika hadithi za Mtume (saw) zilizopokewa na maulamaa wa hadithi wa Shia na Suni. 1075707
captcha