Katika ujumbe huo uliotumwa jana Jumapili, Hamas imeelezea masikitiko yake makubwa kutokana na habari za tukio hilo chungu na kuwatakia subira wajane, familia na jamaa wa mkasa huo.
Katika sehemu nyingine ya ujumbe huo Hamas imewatakia maghfira wahanga wa janga hilo na pia nafuu ya haraka wale wote waliopata majeraha katika tetemeko hilo.
Ni muhimu pia kuashiria hapa kwamba kufuatia mkasa huo wa Azarbaijan Mashariki, mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa wanaofanya kazi nchini Iran wametuma salamu zao za rambirambi kwa Wizara ya Mambo ya Nje wakiilezea masikitiko na maombolezo yao na wananchi wa Iran na kwamba wako tayari kutoa msaada wowote wa kibinadamu kwa waathirika. 1077236