Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Yemen, maonyesho hayo ambayo yamepangwa kuendelea kwa muda wa wiki moja yamefunguliwa na Naibu Gavana wa Taiz katika Taasisi ya Sayansi na Utamaduni ya mkoa huo.
Maonyesho hayo yanayofanyika kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kiutamaduni ya Hail Said An'am ya Yemen yanahudhuriwa na zaidi ya wanakaligrafia na wasanii 15 mashuhuri wa masuala ya uandikaji aya za Qur'ani kwa hati maalumu za mkono.
Muhammad al-Asali, Mkuu wa Nyumba ya Sanaa ya Yemen amesema katika sherehe za ufunguzi wa maonyesho hayo kwamba baadhi ya mabango yanayoonyeshwa kwenye maonyesho hayo ni yale yaliyokusanywa na nyumba hiyo ya sanaa katika warsha mbalimbali za masomo. Muhammad al-Asali ameendelea kusema kuwa maonyesho hayo yameandaliwa kwa ajili ya kuwajulisha watu utajiri mkubwa na wa kale wa Taiz katika masuala ya kaligrafia ya Qur'ani.
Amesema mwishoni mwa hotuba yake kwamba maonyesho kama hayo yamepangwa kufanyika Sanaa mji mkuu wa Yemen baada ya Idul Fitr. 1077488