Kwa mujibu wa tovuti ya emarraked, shere hiyo ilianza mara tu baada ya swala ya Magharib katika Msikiti wa Hassan II mjini Casablanca ambapo inakisiwa kuwa zaidi ya watu laki mbili walishiriki.
Washiriki wa sherehe hiyo walisoma aya za kitabu kitakatifu cha Qur'ani, ama mtu mmoja mmoja au katika makundi. Umati mkubwa wa watu ulishiriki katika sheherehe hiyo kwa kadiri kwamba msikiti na kumbi zake zilijaa na waumini wengi walilazimika kuswali na kusoma kitabu hicho kitakatifu kwenye barabara za pembeni zinazouzunguka msikiti huo.
Vyombo vya habari vya Morocco vimeripoti kuwa sheherehe hiyo ilikuwa kubwa na kwamba haijawahi kushuhudiwa nchini humo kwa kutilia maanani joto kali lililotawala mji huo wakati wa kufanyika sherehe hiyo ya kuhitimishwa Qur'ani Tukufu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi kubwa ya shakhsia wa kidini, kisiasa, kiutamaduni na kimichezo wa nchi hiyo walishiriki katika sherehe hiyo ya kufana. 1078250