Kitengo cha Utamaduni cha Haram ya Abulfadhil Abbas (as) katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq kimeadaa mahafali ya kila siku ya usomaji Qur'ani katika haramu hiyo kutokana na idadi kubwa ya wafanyaziara wa Kiirani wanaozuru haram hiyo na ile iliyo karibu ya Imam Hussein (as).