IQNA

Mbunge ataka kusitishwa uchapishaji wa nakala za Qur'ani nchini Misri

18:36 - August 14, 2012
Habari ID: 2393073
Mbunge mmoja wa Misri ametoa wito wa kusitishwa uchapishaji wa nakala za Qur'ani Tukufu katika viwanda vya uchapishaji ambavyo havisimamiwi ipasavyo.
Wito huo umetolewa baada ya kusambazwa madukani nakala za Qur'ani zenye juzuu 28 na 29 tu za Qur'ani Tukufu.
Mbunge Musa Ali Ahmad aliwasilisha ombi hilo kwa Spika wa Bunge la Misri Ahmad Fahmi akitaka kusitishwa uchapishaji wa nakala za Qur'ani katika viwanda visivyokuwa na usimamizi wa kutosha.
Alisema nakala elfu 40 za Qur'ani zenye juzuu 29 na elfu 40 zenye juzuu 28 zimesambazwa madukani.
Mbunge huyo aliwaonyesha wabunge wenzake nakala za aina hiyo za Qur'ani zenye upungufu wa juzuu na akakitaka kiwanda kikuu cha uchapishaji Qur'ani cha Wizara ya Wakfu ya Misri kusimamia uchapisha wa Qur'ani nchini humo. 1078406

captcha