Chama hicho kimewataka Wamisri kuhudhuria kwa wingi katika mahfali hiyo ya Qur'ani na kutangaza uungaji mkono wako kwa Rais Muhammad Mursi wa nchi hiyo.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin amesema kuwa harakati hiyo na vyama vingine vya kitaifa na kimapinduzi vitashiriki katika mjumuiko huo wa mamilioni ya watu kwa ajili ya kuhitimisha Qur'ani Tukufu ambapo pia vitatangaza uungaji mkono wao kwa maamuzi yaliyochukuliwa na Rais Mursi. 1079459