Shirika la habari la Malaysia Barnama limeripoti kuwa Jumuiya ya Kimataifa ya Ushirikiano wa Kiislamu ya Malaysia (Ikiam) imepewa jukumu la kubuni muundo wa muungano huo.
Uamuzi wa kuanzishwa muungano huo ulichukuliwa katika kikao cha jana cha jumuiya za Kiislamu zisizo za serikali katika nchi za kusini mashariki mwa Asia. Katika kikao hicho ilitajwa kuwa lengo la kuanzishwa muungano huo ni kufanya jitihada za kukomesha mgogoro wa Myanmar na ukatili unaofanyika nchini humo dhidi ya Waislamu katika jimbo la Arakan.
Myanmar pia ni mwanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN). 1079294