IQNA

Wafuasi wa dini mbalimbali waandamana mbele ya msikiti wa California kuwaunga mkono Waislamu

16:03 - August 15, 2012
Habari ID: 2393973
Wafuasi wa dini mbalimbali wamekusanyika mbele ya msikiti wa mji wa Ontario katika jimbo la California huko marekani ambao wiki iliyopita ulishambuliwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.
Wafuasi hao wa dini mbalimbali walitangaza uungaji mkono na mshikamano wao na Waislamu wa mji wa Ontario.
Marshall Leonardo ambaye ni mkazi wa eneo jirani na msikiti huo ameliambia gazeti la Daily Bulletin kuwa Waislamu ni watu wema na kwamba dini ni miongoni mwa mambo ambayo ni sehemu ya uhuru wa mwanadamu ambao unatumiwa na Waislamu kuzungumza na Mungu wao.
Kasisi wa kanisa la Unity la mji wa Pomona katika jimbo la California John Chess amesema: "Awali sikuwa na maarifa yoyote kuhusu dini ya Uislamu lakini baada ya kufanya uchunguzi kuhusu wafuasi wa dini hiyo nimeona kuwa Waislamu ni sawa na wafuasi wa dini nyinginezo na wanaamini misingi kama tunayoimanini sisi."
Baada ya shambulizi la wiki iliyopita dhidi ya msikiti wa mji wa Ontario ambalo ni sehemu ya wimbi la hujuma inayolenga misikiti na vituo vya Waislamu nchini Marekani, polisi ya mji huo ilitangaza kuwa imeanza uchunguzi wa kuwasaka watu waliohusika na shambulizi hilo.
Waislamu wa mji huo wanaamini kwamba shambulizi hilo limekuwa na matokeo kinyume na matarajio ya watekelezaji wake na limekuwa sababu ya kukutana na kuungana zaidi wafuasi wa dini mbalimbali. 1079532



captcha