IQNA

Washindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani waenziwa Algeria

18:40 - August 15, 2012
Habari ID: 2394000
Sherehe ya kuenzi na kuwashukuru washindi wa duru ya tisa ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ilifanyika jana Jumanne katika msikiti mkuu wa mjini Algiers ikihudhuriwa na Rais Abdul Aziz Bouteflika wa nchi hiyo.
Sherehe hiyo ilifanyika kwa lengo la kuwashukuru waandaaji na washindi wa mashindano hayo yaliyopewa jina la Taj al-Qur'ani.
Rais Bourteflika aliwapa zawadi washindi wa kwanza hadi tatu wa mashindano hayo ya kimataifa ambao walikuwa ni kutoka katika nchi za Libya, Bangladesh na Chad kwa utaratibu. Vilevile aliwashukuru waandaaji, wasimamizi na kamati ya waamuzi wa mashindano hayo ya kimataifa.
Mbali na ujumbe wa serikali, mabalozi wa nchi kadhaa za Kiislamu pia walishiriki katika sherehe hiyo.
Wawakilishi wa nchi 50 walishiriki katika mashindano hayo yaliyoanza tarehe 8 Agosti na kukamilika jana Jumanne mjini Algiers.1079364
captcha