Kwa mujibu wa ofisi ya mawasiliano ya umma ya kituo hicho, swala hiyo itasimamishwa katika kituo hicho kuanzia saa mbili asubuhi kwa wakati wa Vienna.
Kituo hicho kimewataka Waislamu wa Austria kuwasiliana nacho kuanzia saa mbili na nusu Jumamosi usiku au kutembelea tovuti yake kwa anwani ifuatayo: www.izia.at ili kujua iwapo hilali ya mwezi wa Shawwal itakuwa imeonekana au la.
Huku kikiwapongeza Waislamu na kuwapa mkono wa heri na fanaka kwa mnasaba huu muhimu, kitengo hicho cha Kiislamu kimetangaza kuwa zakaatul fitr kwa kila Mwislamu nchini humo ni euro 6. 1079324