Kwa mujibu wa uchunguzi huo misikiti 19 ilijengwa katika ufalme huo mwaka uliopita na miwili mwaka huu na hivyo kufanya idadi ya misikiti katika ufalme huo kuongezeka kutoka misikiti 1,043 hadi 1,418.
Hata kama asilimia 34 ya misikiti ya Dubai imejengwa na Taasisi ya Masuala ya Kiislamu na Heri ya Dubai (IACAD) lakini watu, jumuiya na mashirika binafsi pia yamekuwa yakishirikiana na taasisi iliyotajwa katika ujenzi wa msikiti hiyo.
Takwimu zinaoonyesha kwamba misikiti 633 imejengwa katika mtaa wa Dira, 438 katika eneo la Bur Dubai ambapo swala za ijumaa husimamishwa katika asilimia 36 ya misikiti hiyo. 168 kati ya misikiti hiyo kila mmoja una uwezo wa kubeba watu zaidi ya 1000.
Kwa ujumla misikiti ya Dubai ina uwezo wa kutoa huduma kwa waumini laki sita. 1079521