IQNA

Waislamu wa Uingereza kunufaika na mfumo wa fedha wa Kiislamu

12:47 - August 16, 2012
Habari ID: 2394324
Kwa mara ya kwanza Waislamu wa Uingereza wanatarajiwa kunufaika na mfumo wa fedha wa Kiislamu katika miamala yao ya kifedha na kibiashara.
Kwa mujibu wa tovuti ya OnIslam, 'Utaratibu wa Kifedha wa Kiislamu' ni mpango mpya ambao baada ya kuanza kutekelezwa katika mfumo wa benki za Uingereza utawawezesha Waislamu wa nchi hiyo kunufaika na mfumo wa kifedha wa Kiislamu ambao unazingatia sheria za Kiislamu.
Hayo yamesemwa na Shabab Golfaraz, mshauri wa masuala ya kifedha wa mpango ulioatajwa wa fedha alipokuwa akizungumza na gazeti la Uingereza la Yorkshire Post. Amesema huduma nyingi za fedha nchini Uingereza zimesimama juu ya msingi wa riba ambao umeharamishwa na Uislamu.
Amesema mpango huo ambao kwanza ndio umeanza kutekelezwa katika eneo la Yorkshire katika mwezi huu wa Ramadhani utaenezwa baadaye katika pembe zote za nchi hiyo. Ni muhimu kuashiria hapa kwamba Waislamu wapatao milioni 2 hadi 3 wanaishi Uingereza ambapo asilimia 25 hadi 30 kati yao wanaishi katika jimbo la Yorkshire Magharibi.
Uingereza ni nchi pekee ya Ulaya ambayo hadi sasa inaruhusu benki za Kiislamu kutoa huduma zao kwa wateja wao wa Kiislamu. 1079788
captcha