Kwa mujibu wa tovuti ya Muslim Village, Waislamu 35,000 wanaishi katika mji wa Yiwu ambapo nusu ya jamii hiyo ni ya wahajiri kutoka nchi nyingine hasa za Kiarabu.
Mwaka 2004 idadi ya Waislamu wa mji huo iliongezeka sana kadiri kwamba viongozi wa mji huo walilazimika kuwapa Waislamu sehemu ambayo awali ilikuwa imetengwa kwa ajili ya kuanzishwa karakana ya hariri, ili wajenge hapo sehemu yao ya ibada. Msikiti mkubwa wa Waislamu sasa unajengwa katika eneo hilo kwa msaada wa wafadhili wa ndani na nje.
Ushirikiano wa Waislamu na viongozi wa mji huo ni mkubwa kiasi kwamba huwa wanaruhusu barabara za pembeni ya eneo hilo kutumiwa na Waislamu kwa ajili ya ibada zao wakati msikiti huo unaposhindwa kuhimili idadi ya waumini.
Wakati huohuo ongezeko kubwa la Waislamu katika mji huo limeinua kiwango cha uchumi wa mji huo kwa kuwapa wamiliki wa maeneo ya kibiashara pato kubwa na faida za kibiashara. 1079645