IQNA

Mchuano mkali kati ya makarii wa Afghanistan na Qatar katika mashindano ya Qur'ani ya al Kauthar

18:50 - August 18, 2012
Habari ID: 2395833
Usiku wa 29 wa mashindano ya Qur'ani yanayoendeshwa na televisheni ya al Kauthar ya Iran ambayo yamepewa jina la "Inna Lilmuttaqina Mafaza" umeshuhudia mchuano mkali kati ya makarii wa Afghanistan na Qatar.
Awamu hii ya mwisho ya mashindano ya Qur'ani ya al Kauthar inawakutanisha pamoja makarii kutoka nchi za Iraq, Afghanistan, Qatar, Misri na Saudi Arabia.
Majaji wa mashindano hayo yanayorushwa hewani moja kwa moja katika usiku za mwezi mtukufu wa Ramadhani kwenye televisheni ya al Kauthar ni kutoka Iran, Syria, Misri na Iraq.
Mashindano ya Inna Lilmuttaqina Mafaza yanayofanyika katika televisheni ya al Kauthar ya Iran ndiyo mashindano pekee ya Qur'ani yanayofanyika katika ulimwengu wa Kiislamu kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani na mshindi wake wa kwanza atapata zawadi ya dola elfu 5, mshindi wa pili dola elfu 4, mshindi wa tatu dola elfu 3, mshindi wa nne dola elfu 2 na mshindi wa tano dola elfu moja za Kimarekani. 1081493
captcha