IQNA

Maonyesho ya bidhaa halali nchini Japan

18:50 - August 18, 2012
Habari ID: 2395834
Taasisi moja isiyo ya serikali katika mji wa Fukuoka nchini Japan imetangaza kuwa itafanya maonyesho ya kwanza ya bidhaa halali nchini humo mwezi Januari mwakani.
Tovuti ya Japan Times imeripoti kuwa, jumuiya hiyo inasema lengo la maonyesho hayo ni kunyanyua kiwango cha bidhaa za vyakula nchini Japan kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Imeongeza kuwa maonyesho hayo yatazidisha fursa ya kutumwa bidhaa za chakula za Japan katika nchi za Waislamu na kukukidhi mahitaji ya Waislamu wa Japan.
Jumuiya ya Biadhara ya Japan inasema kuwa, maonyesho hayo yatakuwa ya kwanza ya bidhaa halali kufanyika nchini humo.
Maonyesho hayo yatakayosimamiwa na Jumuiya ya Hilali ya Asia nchini Japan yatakuwa na aina karibu 30 za vyakula kutoka viwanda na jumuiya za ushirika za kilimo. 1081577
captcha