IQNA

Karii wa Iran ashinda mashindano ya Qur'ani ya al Kauthar

18:21 - August 21, 2012
Habari ID: 2396681
Karii mashuhuri wa Qur'ani wa Iran Hussain Yazdanpanah ameshinda mashindano ya Qur'ani ya Inna Lilmuttaqina Mafaza yaliyosimamiwa na televisheni ya Iran ya al Kauthar.
Awamu ya mwisho ya mashindano hayo ilitawaliwa na mchuano mkali kati ya wasomaji watano kutoka Afghanistan, Uholanzi, Imarati na Iran.
Majaji wa mashindano hayo walitoka nchi za Iraq, Misri, Syria na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mashindano ya Inna Lilmuttaqina Mafaza yaliyofanyika katika televisheni ya al Kauthar ndiyo mashindano pekee ya Qur'ani yaliyofanyika katika ulimwengu wa Kiislamu kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mshindi wa pili wa mashindano hayo alikuwa Muhammad Amin Wahidi kutoka Iran na watatu alikuwa Ali Muhammad Jawad kutoka Uholanzi. Ali Ridha Ridhai kutoka Afghanistan ameshika nafasi ya nne na Sayyid Nizar al Hashimi kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu ameshika nafasi ya tano.
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Inna Lilmuttaqina Mafaza amepata zawadi ya dola elfu 5, mshindi wa pili dola elfu 4, mshindi wa tatu dola elfu 3, mshindi wa nne dola elfu 2 na mshindi wa tano dola elfu moja za Kimarekani.
Mashindano hayo yalikuwa yakirushwa hewani moja kwa moja na televisheni ya satalaiti ya al Kauthar. 1082032
captcha